Uvumbuzi wa Mbinu ya Mpango wa Kujitolea Wakufichua Iwapo Mtu Amelipa Ushuru (Voluntary Tax Disclosure Programme)

Katika jitihada za kuimarisha ulipa ushuru nchini kenya, Mamlaka ya Kulipa Ushuru Nchini Kenya imepanua njia mbadala ya waliokwepa kulipa ushuru kupitia uvumbuzi wa mbinu ya mpango wa kujitolea wa kufichua iwapo mtu amelipa ushuru kupitia sharia ya kuthibiti fedha 2022, kuanzia tarehe 1 Januari 2021. Hali hii itaendelea hadi Desemba tarehe 31 mwaka wa 2023.

Mpango wa kujitolea wa kufichua iwapo mtu amelipa ushuru inawapa walipa kodi fursa ya kufichua kisiri madeni ya kodi ambazo hazija fichuliwa awali kwa kamishna na nia ya kuweza kurahisishiwa adhabu na riba ya kodi iliyofichuliwa.

Ufichuzi unaostahili kufichuliwa chini ya mpango huo, utakuwa kodi ambazo hazijawekwa hadharani kwa mamlaka  ya kulipa ushuru. Mbali na hayo, madeni ya ushuru ambayo yamekua yakiongezeka kwa kipindi cha miaka mitano tangu tarehe 1 Julai 2015 hadi tarehe 30 Juni 2020, na baada ya hapo kunufaika kutokana na kuondolewa kwa adhabu na riba kuanzia asilimia mia moja, hadi asilimia ishirini na tano za riba zilizokua zimekua zikiongezeka kwa njia ya adhabu na riba

Mpango huo unamhitaji mlipa kodi kufichua kodi kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 1 Januari 2021 hadi 31 Desemba 2023.  Iwapo mlipa kodi ataweza kufichua malipo ya kodi yake katika mwaka wa kwanza wa mpango huo (2021) ya kipindi cha mwaka mmoja, walipa ushuru watapata faida kutoka asilimia mia moja ya adhabu ya riba.Hata hivyo iwapo ufichuzi utafanyika katika mwaka wa pili na wa tatu wa kipindi hicho (2022 na 2023), walipa kodi wanaweza kunufaika kutokana na kupewa msamaha wa asilimia  hamsini na asilimia ishirini na tano ya adhabu na riba zilizoongezeka mtawalia.

Mtu anayetamani kujumlishwa katika mpango huu wa kujitolea kufichua iwapo amelipa ushuru, anastahili kujiunga na mtandao wa masuala ya ushuru , aingize neno siri na neno siri yake binafsi, ateue sehemu ya Mpango wa kujitolea kufichua ushuru chini ya mapato yanayotokana na kodi.

Walipa kodi wataitajika kuchagua wajibu wa kulipa ushuru. Wanaoona haja ya kutoa ombi la kusamehewa kutokana na deni la ulipa kodi, wabonyeze kitengo chenye kipindi cha kufanya jumla ya kodi anazostahili kulipa, kisha aongeze stakabathi zinazoonyesha masuala ya kodi, ajumlishe mapato ambayo hakuweza kutangazia tume na maeneo yote ambayo ni lazima kisha awasilishe ombi hilo.

Ombi litaweza kukubaliwa mtu anapotuma ombi lake katika ofisi ya ulipaji ushuru. Mlipa ushuru ataweza kutoa malipo tu iwapo ombi lake limekubaliwa 

Iwapo ombi litakubaliwa au litakataliwa, mlipa kodi atapata jawabu la kukubaliwa au kukataliwa kwa njia ya ujumbe wa barua pepe. Wale waliokubaliwa wataweza kunakili risiti kulingana na kitengo cha mpango wa kujitolea kufichua iwapo amelipa ushuru na kisha atolee malipo kulingana na maagizo na kisha cheti cha VTDP kutolewa 

Watu waliopewa chini ya VTDP hawatashtakiwa kwa madeni ya kodi yaliyofunguliwa chini ya kipindi hicho. Anayeomba kupewa fursa ya kupewa utulivu wa madeni yao ya kodi yaliyofunguliwa kwa awamu kama alivyoungana na kamishna. Hata hivyo, mtumizi wa masuala ya ushuru anapokosa kutangazia tume masuala ya ukweli, kamishna ana uhuru wa kukataa kumpa wepesi wa malipo pamoja na ushuru au hata ana uwezo wa kuanzisha mashtaka.

Hata hivyo, walipa kodi hawatapewa uhuru wa mamlaka ya kulipa ushuru iwapo yupo chini ya ukaguzi, uchunguzi au umuhimu wa kodi.Walipa kodi watazuiliwa kutokana na kunufaika na VTDP ikiwa kamishna wa masuala ya ushuru na ulipa kodi wa jumia hajawaarifu kuhusu ukaguzi ambao haujakamilika ama uchunguzi

Baada ya muda mrefu inataragiwa ya kuwa VTDP itawashawishi vyema wananchi hali ya ulipa kodi kwa njia inayostahili miongoni mwa watu nchini na kuongoza ukusanyaji wa ushuru wakati ule kipindi kipo katika utendekazi wao

BY : ELMAD KOYO


BLOG 22/06/2022


Did you find this content useful?

Average Rating

5
Based on 1 rating
💬
Uvumbuzi wa Mbinu ya Mpango wa Kujitolea Wakufichua Iwapo Mtu Amelipa Ushuru (Voluntary Tax Disclosure Programme)