Stempu za Ushuru kwenye Maji ya Chupa, Juisi, Soda, Vinywaji na Vipodozi vingine visivyo na kileo.

Mamlaka ya Mapato ya Kenya inapenda kuwafahamisha watengenezaji, waagizaji na umma kwamba Mfumo wa Kusimamia Bidhaa Zinazoweza Kutozwa Ushuru kwenye maji ya chupa, juisi, soda, vinywaji vya kuongeza nguvu na vinywaji vingine visivyo na kileo, na vipodozi ambao uliratibiwa kufanyika 1.st Septemba, 2019 imeahirishwa ili kuruhusu watengenezaji kukamilisha usakinishaji. Tarehe mpya ya Go-Live itawasilishwa kwa wakati ufaao.

Ukihitaji ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana nasi kwa Barua pepe: ushiriki.wadau@kra.go.ke; callcentre@kra.go.ke  au tafadhali piga simu kituo chetu cha mawasiliano kwa Simu: (0) 20 4 999 999; 0711 099 999

 

Kamishna wa Ushuru wa Ndani

 


ANGALIZO KWA UMMA 30/08/2019


💬
Stempu za Ushuru kwenye Maji ya Chupa, Juisi, Soda, Vinywaji na Vipodozi vingine visivyo na kileo.