Stempu za ushuru bandia zakamatwa katika kampuni ya maji ya Limuru

Kukamatwa kwa gari lililokuwa na maji ya chupa yaliyobandikwa stempu ghushi katika eneo la Kanyonyo kaunti ya Kitui kumesababisha kugunduliwa kwa stempu zaidi za thamani ya Kshs. 850,000 katika mapato katika kiwanda cha maji kilichopo Limuru.

Gari lililokuwa likisafirisha maji ya Farris Pure Natural Spring likiwa na stempu ghushi lilinaswa na Timu ya Multi Agency (MAT) tarehe 11 Julai 2020.

KRA ilifuatilia chanzo cha stempu hizo kwa Montana Supplies Limited, kiwanda cha kujaza maji katika eneo la Tigoni, Limuru na kugundua stempu 42,672 ambazo ni ghushi na zilizopatikana kinyume cha sheria.

Timu ya Multi Agency ilinasa na kulizuilia gari hilo katika kituo cha polisi cha Mwingi ambapo KRA ilifanya uhakiki wa 100% kwenye stempu za chupa za maji na kugundua chupa 5940 za lita 1.5 za chapa ya maji ya Farris Pure Spring zikiwa zimebandikwa stempu ghushi na chupa 7392 za lita 1.5 bila mihuri ya ushuru.

Chupa hizo za maji zilikuwa zimefichwa ndani ya lori chini ya shehena ya chupa za maji za chapa sawa na zikiwa na stempu halisi za ushuru. Uchunguzi zaidi wa KRA katika kiwanda cha kutengeneza chupa za maji ulipelekea kupatikana kwa stempu hizo ghushi. Pia zilizopatikana kutoka kiwandani ni safu ya stempu za ushuru ghushi zilizotumika ambazo hazikutumika.

Wakurugenzi wawili wa kampuni hiyo Idris Ahmed Boru na Garat Hassan Issack, tarehe 31 Agosti walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Milimani Muthoni Nzibe kukabiliwa na shtaka la kukutwa na stempu feki za ushuru na lingine la kupata stempu za ushuru kinyume cha sheria. Tozo zote mbili ni ukiukaji wa sehemu za Kanuni za Ushuru wa Bidhaa (Mfumo wa Kudhibiti Bidhaa Zinazoweza Kulipiwa) za 2017.

Wawili hao walikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu ya Shilingi laki moja (Ksh.100,000) hadi kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi hiyo. Kesi hiyo itatajwa tarehe 17 Septemba 2020. Iwapo watapatikana na hatia, washtakiwa hao watatozwa faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Kamishna, Uchunguzi na Utekelezaji

 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 02/09/2020


Je, ulipata maudhui haya kuwa muhimu?

wastani Rating

5
Kulingana na ukadiriaji 1
💬
Stempu za ushuru bandia zakamatwa katika kampuni ya maji ya Limuru