KRA inaanza kulipa marejesho ya VAT ya Ksh.10 bilioni kwa mashirika ya biashara

Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) imeanza kulipa Ksh.10 bilioni kama marejesho ya VAT kufuatia agizo la rais na kutolewa kwa fedha na Hazina ya Kitaifa.

 

"Tumeanza kulipa mashirika mbalimbali marejesho ya VAT kutoka kwa fedha maalum zilizotolewa na serikali na kutolewa kwa KRA na tunatarajia kukamilisha mchakato wa malipo katika Wiki moja", alisema Kamishna wa Ushuru wa Ndani Bi Elizabeth Meyo.

 

Marejesho hayo yanatarajiwa kutoa unafuu wa kifedha kwa biashara zilizoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 haswa sekta ya kilimo cha bustani, uchukuzi na ukarimu wa uchumi.

 

 "Ni mashirika ya biashara ambayo madai yao ya kurejeshewa yamethibitishwa kwa kufuata taratibu ndio yatapokea malipo," alisema Bi. Meyo.

 

 

 

Kamishna wa Ushuru wa Ndani-Elizabeth Meyo


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 30/05/2020


Je, ulipata maudhui haya kuwa muhimu?

wastani Rating

1.5
Kulingana na ukadiriaji 2
💬
KRA inaanza kulipa marejesho ya VAT ya Ksh.10 bilioni kwa mashirika ya biashara