Walipakodi wahimizwa kufikia huduma za KRA mtandaoni

Mamlaka ya Ushuru nchini (KRA) imeweka mikakati kuwezesha huduma za ushuru kwa umma kutokana na janga la Ugonjwa wa Virusi vya Corona (COVID-19).

Ili kupunguza msongamano katika Ofisi za Huduma ya Ushuru ya KRA, walipa kodi wanahimizwa kufikia huduma za KRA kupitia majukwaa ya mtandaoni.

Huduma zote za Ushuru wa Ndani zinaweza kufikiwa kupitia https://itax.kra.go.ke/KRA-Portal/ huku huduma zinazohusiana na Forodha zinaweza kufikiwa kupitia Mfumo wa Kusimamia Ushuru wa Forodha (iCMS).

Ili kuepusha hatari ya kusambazwa kwa njia ya kushughulikia pesa, KRA pia inahimiza walipa kodi kufanya miamala yote kupitia pesa za rununu.

Mamlaka pia imeweka vitakasa mikono katika Ofisi zote za Huduma ya Ushuru na itahakikisha kuwa majengo yote yanasafishwa mara kwa mara na kutiwa dawa.

KRA inasalia kuwa mojawapo ya mashirika ya serikali ambayo hutoa huduma muhimu na itaendelea kuhudumia umma huku ikiweka usalama wa walipa kodi kwanza.

 

Naibu Kamishna, Masoko na Mawasiliano


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 17/03/2020


Je, ulipata maudhui haya kuwa muhimu?

wastani Rating

2
Kulingana na ukadiriaji 4
💬
Walipakodi wahimizwa kufikia huduma za KRA mtandaoni