Hakuna Usumbufu wa Huduma katika KRA

Mamlaka ya Ushuru nchini (KRA) inawahakikishia walipa ushuru kwamba hakuna kutatizwa kwa huduma katika utendakazi wake wote.

Kama ilivyoelezwa na bodi ya KRA, katika taarifa iliyotolewa tarehe 14th Mei 2019, KRA inawahakikishia walipa ushuru kwamba shughuli zinaendelea bila kukatizwa. Madai ya 'wafanyakazi kwenda polepole' hayawezi kuthibitishwa, kwa kuwa shughuli zote za Ushuru wa Forodha na Ndani zinaendelea. 

Mfumo wa iTax unafanya kazi na walipa kodi wanapaswa kuendelea kuwasilisha marejesho yao na kufanya malipo.

Kwa aina yoyote ya usaidizi kuhusu huduma za KRA, walipa kodi wanahimizwa kupiga simu kituo cha mawasiliano cha KRA kwa nambari 020 4999 999, 0711 0999,999 au kutuma barua pepe kwa callcentre@kra.go.ke. Unaweza pia kutembelea ofisi ya KRA iliyo karibu nawe au Huduma kwa usaidizi zaidi.

 

 

 

Naibu Kamishna, Masoko na Mawasiliano


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 29/05/2019


Je, ulipata maudhui haya kuwa muhimu?

wastani Rating

💬
Hakuna Usumbufu wa Huduma katika KRA