KRA kukusanya KShs.1.4 Bilioni kutoka kwa muuzaji wa jumla wa mchele

Mahakama ya Rufaa ya Ushuru (Mahakama hiyo) imetupilia mbali Rufaa iliyowasilishwa na Jhulay LAL Commodities Ltd kwa misingi kwamba kampuni hiyo imeshindwa kuthibitisha kwamba tathmini ya Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) ilikuwa ya kupita kiasi. Shughuli kuu ya Jhulay LAL ni uuzaji wa jumla na reja reja wa mchele unaotolewa kutoka Pakistani.

Jhulay LAL Commodities Ltd ilikata rufaa dhidi ya uamuzi wa KRA ikipinga ushuru wote wa Kshs. 1,456,433,604.00 zinazodaiwa. Sababu kuu za rufaa hiyo ni kwamba Kamishna aliamua mapato yanayotozwa ushuru kwa misingi ya jumla ya benki zake dhidi ya kanuni za msingi za uhasibu na sheria ya kodi.

KRA ilifaulu kujitetea kuwa ilifanya tathmini hiyo baada ya uchunguzi kufichua dosari kadhaa zikiwemo amana za benki ambazo hazijaelezewa na kwamba mauzo ya mchele huo yalizidi kiasi kilichoagizwa kutoka nje.

Mahakama ilikagua ushahidi kama ulivyowasilishwa na pande zote mbili na ikashikilia kuwa KRA ilitumia mamlaka yake kwa busara kufanya uamuzi kulingana na nyenzo zilizo mbele yake. Mahakama ilisema kuwa Jhulay LAL Commodities Ltd ilishindwa kuthibitisha kwamba tathmini ilikuwa nyingi na ikatupilia mbali rufaa hiyo.

Kamishna, Huduma za Sheria na Uratibu wa Bodi-Bw. Paul Matuku


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 25/05/2021


Je, ulipata maudhui haya kuwa muhimu?

wastani Rating

💬
KRA kukusanya KShs.1.4 Bilioni kutoka kwa muuzaji wa jumla wa mchele