Watengenezaji wa Majengo ya Uchina Wakamatwa kwa Kukwepa Ushuru

Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) imewakamata wakurugenzi watatu wa kampuni ya mali isiyohamishika ya raia wa Uchina kwa kukosa kutangaza na kutuma ushuru wa Ksh.26 milioni.  

Uchunguzi wa KRA ulibaini kuwa watatu hao ambao ni wakurugenzi wa Tianyi Limited-kampuni ya mali isiyohamishika ya nyumba za makazi huko Athi River inayojulikana kama River Park Estate, walishindwa kutangaza na kutuma ushuru wa Kshs. milioni 26 kutokana na mauzo ya vipande mia moja sabini na moja (171). 

Watengenezaji Zhang Xiaodong, Ming Zhao, He Youging walikamatwa Nairobi na wako nje kwa dhamana ya pesa taslimu ya Kshs. 100,000. Watafikishwa mahakamani tarehe 14th Oktoba, 2019.

 

Kamishna wa Uchunguzi na Utekelezaji

 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 09/10/2019


Je, ulipata maudhui haya kuwa muhimu?

wastani Rating

4.3
Kulingana na ukadiriaji 3
💬
Watengenezaji wa Majengo ya Uchina Wakamatwa kwa Kukwepa Ushuru