Mtoa huduma wa kaunti aliyeshtakiwa kwa kukwepa kulipa ushuru wa Sh milioni tatu

Mfanyibiashara aliyetengeza vifaa vya thamani ya Kshs 65 milioni kwa Kaunti ya Trans Nzoia ameshtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Eldoret Mhe. Naomi Wairimu na ulaghai wa ushuru wa Kshs.3 milioni.


Mkurugenzi wa Africonnect Limited Joab Lumbasi Simiyu anakabiliwa na mashtaka manne kwa pamoja na kampuni hiyo. Alikabiliwa na mashtaka mawili ya kushindwa kulipa VAT ya Kshs 2.9 milioni na Kshs 155,000 kwa mwaka wa 2015 na 2016 mtawalia kwa tarehe zilizowekwa. Pia alikabiliwa na makosa mawili ya kushindwa kuwasilisha marejesho ya kodi kwa miaka miwili kama inavyotakiwa chini ya Sheria ya Taratibu za Ushuru ya 2013.


Washtakiwa walikana mashtaka yote na waliachiliwa kwa bondi ya Kshs.100, 000 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.


Tathmini ya ushuru ya KRA kwa mlipa ushuru-Africonnect Limited iligundua kuwa kampuni hiyo ilikuwa imepewa zabuni na Serikali ya Kaunti ya Trans Nzoia na ililipa pesa za jumla ya Kshs 65,000,000 kwa usambazaji wa mitambo miwili ya kuchimba visima kila moja kwa Kshs 33,500,000. Africonnect Limited ilitekeleza zabuni na kulipwa lakini haikuwasilisha marejesho ya VAT wala kulipwa kodi inayodaiwa.


Kesi itasikizwa tarehe 1 Februari 2021. Kwa mashtaka mawili ya kwanza ya kushindwa kulipa kodi, ikiwa mshtakiwa atapatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyozidi Kshs 10,000,000 au mara mbili ya kodi aliyokwepa kwa kiwango chochote kilicho juu au kifungo kisichozidi miaka 10, au vyote kwa pamoja.


Kwa mashtaka ya kushindwa kuwasilisha marejesho ya kodi, mshtakiwa akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyozidi Kshs 1,000,000 na kifungo kisichozidi miaka 3 au vyote kwa pamoja.

 

Kamishna, Uchunguzi na Utekelezaji


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 24/12/2020


Je, ulipata maudhui haya kuwa muhimu?

wastani Rating

💬
Mtoa huduma wa kaunti aliyeshtakiwa kwa kukwepa kulipa ushuru wa Sh milioni tatu