Malipo ya Madeni yote ya Kodi Yanayodaiwa

Katika kipindi hiki kigumu, serikali ilianzisha hatua mbalimbali za kupunguza ushuru ili kuwaepusha Wakenya dhidi ya athari za janga la COVID-19 na kuimarisha uthabiti wa uchumi. Hata hivyo, uhamasishaji wa mapato ya kodi unasalia kuwa kipengele muhimu katika kukamilisha juhudi za serikali katika kuendeleza maendeleo ya nchi yetu.

Kwa hivyo, KRA inawashauri walipa kodi wote walio na dhima za ushuru na hawajalipa au kuingiza mipango ya malipo ya kufanya hivyo kufikia tarehe 20 Juni 2020, bila ambapo hatua zifaazo za utekelezaji zitachukuliwa dhidi ya deni ambalo halijalipwa. Walipa kodi walioathiriwa wanashauriwa kuwasiliana na Ofisi ya Huduma ya Ushuru ili kulipa madeni yao ya kodi au kupendekeza mipango ya malipo.

Kufuatia toleo letu la awali la kuhimiza kukaguliwa kwa mipango ya malipo, KRA inapenda kuwashukuru walipa ushuru wote ambao walipitia mipango yao na wameendelea kuiheshimu.

Kwa ufafanuzi zaidi na uwezeshaji, tafadhali wasiliana na Kituo cha Mawasiliano kwa Simu: 020 4 999 999, 0711 099 999 au Barua pepe. callcentre@kra.go.ke.

 

Kamishna wa Ushuru wa Ndani

 


ANGALIZO KWA UMMA 17/06/2020


💬
 Malipo ya Madeni yote ya Kodi Yanayodaiwa