Uwasilishaji wa Marejesho ya Kodi ya Mapato ya 2019

Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) inawakumbusha walipa kodi wote kwamba marejesho ya ushuru kwa mwaka wa Mapato 2019 yanastahili kuwasilishwa kuanzia tarehe 1 Januari, 2020 hadi 30 Juni, 2020.

Walipakodi wanashauriwa kuzingatia muda na matamko sahihi katika marejesho yao kando na kulipa kodi zote zinazodaiwa.

Waajiri wamehimizwa kutoa fomu za P9 za mwaka wa 2019 kwa wafanyikazi wao wote ili kuwawezesha kuwasilisha marejesho yao.

Walipa kodi wote wanaweza kulipa kodi zao na kuwasilisha marejesho yao ya kodi kwa kuingia kwenye itax.kra.go.ke kwa urahisi wao.

Kwa usaidizi zaidi, tafadhali wasiliana nasi kwa Simu: +254 (020) 4999 999, Simu: +254 (0711) 099 999, Barua pepe: callcentre@kra.go.ke au tembelea Kituo chetu chochote cha Usaidizi kote nchini. 

Kamishna wa Ushuru wa Ndani


ANGALIZO KWA UMMA 27/01/2020


💬
Uwasilishaji wa Marejesho ya Kodi ya Mapato ya 2019