Kuhusu KRA
Sisi
ni Nani
Mamlaka ya Mapato, Kenya, ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura ya 469 ya sheria za Kenya, ambayo ilianza kutumika tarehe 1 Julai 1995. KRA inajukumu la kukusanya ushuru kwa niaba ya serikali ya Kenya
Majukumu ya msingi ya Mamlaka ni:-
- Kutathmini,Kukusanya na kuwajibika kwa ushuru kwa mujibu wa sheria zilizoandikwa na Masharti maalum ya sheria zilizoandikwa.
- Kushauri juu ya maswala yanayohusiana na usimamizi, na ukusanyaji wa mapato chini ya sheria zilizoandikwa au masharti maalum ya sheria zilizoandikwa.
- Kutekeleza majukumu mengine yanayohusiana na ushuru kama waziri atakavyoelekeza.
Majukumu yetu ya Kimsingi
Ukusanyaji wa Ushuru
Uwezeshaji wa Biashara
Udhibiti wa mipaka
Dira, Dhamira na Maadili
Dira
Mamlaka inayoaminika kimataifa kuwezesha utiifu wa kodi na forodha.
Dhamira
Kuimarisha uhamasishaji wa mapato ya Serikali na kuwezesha ukuaji wa shughuli za kiuchumi na biashara kwa kuhakikisha uzingatiaji wa sheria za kodi na forodha.
Maadili
Anayeaminika, Mwenye Maadili, Mwenye Uwezo, Mwenye Msaada, Rahisi